Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ujumbe wa watumishi wanawake kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) leo Machi 8, 2025 umetembelea mahabusu ya watoto Upanga jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Mwenyekiti wa THTU tawi la TEWW ambaye aliongoza ujumbe huo, Bi. Silyvia Shengena alimkabidhi Meneja wa mahabusu hiyo, Bwana Darius Kalijongo vitu vyenye thamani ya jumla ya Shs. 500,000/=, vikijumuisha: Sabuni za maji, mafuta ya kula na sukari.
Vitu vingine ni: viberiti, mchele, juice, tambi na mafuta ya kupaka.
Akiongea baada ya kupokea msaada huo, Bwana Kalijongo uliushukuru ujumbe huo kwa ukarimu wao na kuwaombea baraka za Mungu.
Mwaka huu kilele cha maadhimisho ya Siku wanawake duniani yamefanyika kimkoa viwanja vya Leaders wilayani Kinondoni jijini Dar es Salam ambapo wanawake hao wa TEWW walishiriki pia.