Baadhi ya watumishi wanawake wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Makao makuu, Dar es Salaam wakiwa katika maandamano leo Machi 8, 2025, viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam kuadhimisha Siku ya wanawake duniani.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ya kimkoa yaliyobeba Kauli mbiu isemayo "Wanawake na wasichana tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji" alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila.