TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
(TEWW)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
KUTOA MAONI JUU YA MABORESHO YA SHERIA YA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (SHERIA NAMBA 12 YA MWAKA 1975)
KUTOA MAONI JUU YA MABORESHO YA SHERIA YA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (SHERIA NAMBA 12 YA MWAKA 1975)
12th Jun, 2024

TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (llianzishwa kwa Sheria Na.12 ya 1975) Simu' Na: +255-222150838 /2151048 Barua pepe: info@iae.ac.tz Tovuti: www.iae.ac.tz Kumb. Na: lAE/LA.292/597 tw .SSstimfi `RTng S.L.P. 20679, Mtaa: Blbi Titi Mohammed Msimbo Na. 23 11102 DAR ES SALAAM TANZANIA. Tarehe: 01/07/2024 WADAU WOTE WA ELIMU, TANZANIA. YAH: Ku_TOA MAONI JUU YA MABORESHO YA SHERIA YA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (SHERIA NAMBA 12 YA MWAKA 1975) Rejea kichwa cha habari hapo juu. 2. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni Taasisi ya Serilkali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria Namba 12 ya mwaka 1975 (Sheria ya Elimu ya Watu Wazima, Sura ya 139) ambapo pamoja na mambo mengine inajishughulisha na kutoa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasimi, kutoa mafunzo ya kozi mbalimbali kwa walimu wa elimu ya wa{u wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. 3. Napenda kukutaarjfu kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TE\/\/\/\/) kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekusudia kufanya maboresho ya sheria iliyoanzisha Taasisi. Hivyo, TE\/V\/V imeandaa bango kitita kuonesha maeneo ambayo yanakusudiwa kuboreshwa. Ili maboresho hayo yaweze kupata idhini ya Bunge, ni vyema wadau wakatoa maoni, ushauri na mapendekezo katika maeneo yaliyoainishwa pamoja maeneo mengineyo ambayo hayajaguswa katika mapendekezo ya mabadiliko ya sheria tajwa. Mawasiliano ya kiofisi yaelekezwe kwa Mkuu wa Taasisi, Nukuu ya Kumb.Na. ni muhimu 4. Miongoni mwa maeneo yanayopendekezwa kufanyiwa maboresho/mabadiliko ni Jina la Taasisi na Cheo cha Kiongozi Mkuu wa Taasisi. Inapendekezwa kwamba Cheo cha Mkuu wa Taasisi kiwe Mkuu wa Chuo (Rector) badala ya Mkurugenzi (Director) na jina la Taasisi libadilike kutoka `Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima' kuwa moja kati ya majina yafuatayo;- i. Tanzania Institute of Life Long Learning (TILL ) -Taasisi ya Elimu bila ukomo, ii. Institute ofAdultand Non-Formal Education (lANFE) -Taasisi ya Elimu yawatu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi. iii. Institute of Adult and Continuing Education (lACE) - Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu. 5. Pamoja na barua hii, nimeambatisha nakala ya bango kitita pamoja na nakala mtandao ya sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ili muweze kupitia na kutoa maoni na ushauri ili kuboresha sheria hii. Tutashukuru iwapo maoni na ushauri wa maboresho ya sheria hii yatawasilishwa makao makuu ya TEWW, kabla au ifikapo tarehe 15 Julai, 2024, kupitia anuani jfuatayo: Mkuu wa Taasisi, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Barabara ya Bibi Titi Mohamed, Msimbo Na. 23, S.L.P 20679, Dar es Salaam, Simu Na. +255 22 2150838/2151048, 0750 292 847 Barua pepe: info@iae.ac.tz, 6. Ni matumaini yangu kuwa utatoa maoni na ushauri ili kuboresha sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa maendeleo ya elimu nchini. 7. Nashukuru kwa ushirikiano wako endelevu. Dkt. P KAIMU fvIKUU WA TAASISI yYaA;T#prprThw#kJ#-A:ZTjIT.~aFi !&hl mr}.h At3} r". :in i/I h irn I I "kuu wa l]aasis