Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa wawakilishi wa wahitimu wa Shahada ya Uzamili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Machi 27, 2025 ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wahitimu hao aliowahi kuwafundisha akiwa Mkufunzi chuoni hapo walitoa tuzo hiyo kutambua mchango wake katika kuendeleza elimu ya watu wazima nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Bi. Emmanuela Kaganda (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga (wa pili kushoto) wakimsikiliza mmoja wa washiriki wa maonesho ya bidhaa bunifu zilizobuniwa na walimu wa Programu ya Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA), viongozi hao walipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa kilele cha kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa programu ya IPOSA. Maonesho hayo ya siku moja yaliyofanyika mjini Babati Machi 14, 2025 yalizishirikisha halmashauri saba za Mkoa wa Manyara.
Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Zacharia Mganilwa (aliyekaa, kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kuhitimisha kikao chao cha kawaida makao makuu ya ofisi za TEWW jijini Dar es Salaam. Wa tatu (kutoka kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Dkt. Lulu Mahai, na aliyekaa (kulia) ni Katibu wa Baraza na Mkuu wa TEWW, Prof. Philipo Sanga.
Baadhi ya Viongozi Waandamizi kutoka Idara ya Magereza na TEWW wakifuatilia mjadala wakati wa mazungumzo kuhusu mashirikiano baina ya Taasisi hizo leo Agosti 19, 2024.
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Mussa Ramadhani Sima (Mb), akipokea Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma unaotumiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika kutekeleza majukumu yake wakati wa ziara ya Kamati hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 20 Januari 2024.
Prof. Philipo Lonati Sanga
Mkuu wa Taasisi
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE) ilianzishwa mwaka 1960 kama kitengo cha masomo ya nje ya darasa cha Chuo cha Makerere, chini ya Chuo Kikuu cha London. Mnamo mwaka 1963, Taasisi hiyo iliboreshwa...