Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko (mwenye ushungi) akiongozana na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi (mwenye suti), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon (wa kwanza kulia) na wajumbe wa kamati wakiondoka katika kituo cha TEWW mara baada ya kukagua kituo hicho kilichopo mjini Kibaha, Pwani leo Septemba 11, 2024.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya Sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP-AEP) Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara katika kituo cha Taasisi hiyo mjini Kibaha, Pwani leo Septemba 11, 2024.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi (katikati) na viongozi wengine (waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo waliopandishwa madaraja hivi karibuni mara baada ya mkutano wa wafanyakazi wote wa TEWW walioko jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika makao makuu ya TEWW mtaa wa Bibi Titi Mohamed jijini Dar es Salaam, leo Agosti 22, 2024.
Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Naibu Mkuu wa Taasisi (Mipango, Fedha na Utawala), Dkt. Godfrey Mnubi (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti, Machapisho na Ushauri Elekezi, Dkt. Bellingtone Mariki (wa pili kushoto) wakifuatilia wasilisho la Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Michael Ng’umbi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa TEWW walioko jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 22, 2024 makao makuu ya TEWW mtaa wa Bibi Titi Mohamed jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi akiongea wakati wa mkutano wa wafanyakazi wote wa taasisi hiyo walioko jijini Dar es Salaam (hawako pichani) leo Agosti 22, 2024, makao makuu ya TEWW mtaa wa Bibi Titi Mohamed jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi Waandamizi kutoka Idara ya Magereza na TEWW wakifuatilia mjadala wakati wa mazungumzo kuhusu mashirikiano baina ya Taasisi hizo leo Agosti 19, 2024.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng'umbi (kushoto) akiongoza kikao kilichojadili mashirikiano
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng'umbi (katikati) na Kamishna wa Magereza, Nicodemus Tenga (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa TEWW na Idara ya Magereza Tanzania mara baada ya kikao cha kujadili mashirikiano baina ya Taasisi zao, kilichofanyika leo Agosti 19, 2024 Makao Makuu ya TEWW, mtaa wa Bibi Titi Mohamed, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wakati wa Kongamano la Kitaifa la Elimu bila Ukomo, lililofanyika tarehe 1 Machi, 2024.
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Mussa Ramadhani Sima (Mb), akipokea Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma unaotumiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika kutekeleza majukumu yake wakati wa ziara ya Kamati hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 20 Januari 2024.
Prof. Michael W. Ng'umbi
Mkuu wa Taasisi
Karibuni sana TEWW ni sehemu nzuri ya kufanyia kazi